ahmashmatasi
Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from ahmashmatasi, Health/Beauty, Dar es Salaam.
09/06/2022
Asalamu alaykum
Ndugu zangu tusipeane mtihani
Sio kila anaeota anafanya tendo la ndoa anajini mahaba
Kuna wanaoota kwasababu ya kukua (baleghe)
Kuna wanaoota kwakuwa hawajashirikibtendo la ndoa kwa muda mrefu
Kuna wanaoota km ndoto ya kawaida tuu (aghalabu huwa na maana ya mafanikio au furaha kwa kadri ya vile atakavyofurahi ktk ndoto)
Sio umeota tuu tendo la ndoa basi nna jini mahaba naomba dawa mambo hayawi hivyo jamani
Usije kutibiwa ukajifanya nawewe tabibu
27/12/2020
Life is full of tests, each and every day you are tested, sometimes you pass, sometimes you fail, all that matters is that you learn.
💪🏿💪🏿💪🏿
02/09/2020
Asalamu alaykum warahmatullahi wabarakaatuh
Usiyasahau mauti maana hata ukiyasahau yenyewe yanakukumbuka
Vyovyote iwavyo iposiku utakua maiti
Cheo nguvu elimu ukubwa mamlaka pesa vyote haviwezi kuzuia umauti
Jiandae muda wowote unaweza kuwa maiti
Tekeleza wajibu wako kwa muumba wako maana ndio njia pekee ya kusalimika kabla na baada ya mauti
20/08/2020
Asalamu alaykum warahmatullahi wabarakaatuh
Mola ajaalie mwaka 1442 hijria uwe mwaka wa kheri na izzah kwa umma wa kiislamu
Mola atupe nguvu ya kubaki ktk haki hadi mwisho wa uhai wetu bila kukhofu mitihani na lawama za wenye kulaumu
02/08/2020
ASALAMU ALAYKUM WARAHMATULLAHI WABARAKAATUH
NI BORA UKASAMEHE KULIKO KUHUKUMU KWA MAKOSA
Wengi leo wanajuta kwa maneno ama matendo walioyafanya kwa dhana mbaya
Kila mtu hutazama mambo kwa kipimo chake huenda jambo uliloona ni kosa kwa mtazamo wa mtu mwingine hakuona kua ni kosa aidha kwa kutofahamu ama kwa mazingira aliyopo
Pamoja na kua kutokujua kosa hakukufanyi kutokua mkosefu Jitahidi kujua uhalisia wa jambo kabla ya kulitolea maamuzi maana majuto hua mjukuu na mwenye kuonewa hasahau hujitahidi kuvumilia tuu
Mhukumu mtu kwa kiwango cha kosa lake na k**a huna hakika juu ya kosa lake ni bora ukasamehe
Jitahidi kupunguza mizigo ya matatizo kwa kusamehe na kuwa na hakika na maamuzi yako ili usiwaumize wengine kwa makosa yasiokua yao
#0653732303
12/07/2020
Asalamu alaykum
Ikiwa uwepo wako na kutokuwepo kwako hakuna tofauti jua wewe ni maiti unaetembea
Badilika kuwa mtu mwenye faida kwa umma
.abdallah
#0653732303
10/07/2020
ABU HESHIMA HAILAZIMISHWI
Ni miongoni mwa maneno nilioyapata toka kwa mzee wangu mlezi wangu baba yangu ambae alipenda sana kuniita ABU
Naam heshima hailazimishwi huja kikawaida kulingana na namna ya maisha yako
Mwanao atakuheshimu kulingana na vile unavyoishi nae
Kadhalika ndugu jamaa na marafiki majirani na hata wafanyakazi wenzako ama washirika watakuheshimu kulingana na vile unavyoishi
Ukiwa mlevi utapewa heshima anayostahiki mlevi
Ukiwa mwizi kadhalika utapewa heshima kwa misingi ya wizi
Ukiwa mchamungu utapewa heshima kwa misingi hio n.k
Kamwe usilazimishe kuheshimiwa watu watakupa heshima kulingana na vile wanavyokuchukulia
Usilazimishe watu wakuheshimu utajiingiza ktk msongo wa mawazo bali ishi maisha ambayo unatakiwa kuishi utapata watakao kuheshimu na kukuthamini sana kwa vile ulivyo
Na ni hatari kubwa sana kuigiza maisha ili upate kuheshimika itakupa tabu ktk maisha yako maana utaishi kwa hofu na mashaka kila unapotaka kuwa ktk maisha yako halisi
Usihofie baadhi ya watu kukucheka na kukudharau maana vyovyote iwavyo watu wataendelea kukusema vibaya tuu
lakini punguza hofu maana MRUSHA TOPE HUMRUDIA
Mola akughufirie zambi zako mzee wangu na aifanye kaburi yako kuwa bustani ktk bustani za peponi SHEKH KAMBI RAMADHANI MATASI haupo nasi lakini maneno yako bado yanaishi ktk nafsi zetu
*oudkipanya
#0653732303
08/07/2020
MFANO WAKO NI WENGI
Moja ya walimu zangu alinihadithia wakati anaelekea ma*omoni nchini misri aliona bango limeandikwa مثلك كثير MFANO WAKO NI WENGI
Ni maneno mafupi lakini yana maana kubwa
Yaani ukiwa msomi basi wapo wa*omi wengi mfano wako
Ukiwa muhuni wapo wengi mfano wako
Ukiwa mlevi pia wapo wengi mfano wako
Ukiwa fundi wapo wengi mfano wako
Alayhaal vyovyote utakavyokua wapo wengi km wewe
Nilipotazama maneno ya Allah NAJUU YA KILA MJUZI KUNA MJUZI ZAID
Nikafahamu kua vyovyote utakavyokua kuna watu mbali ya kuwa km wewe bali wamekuzidi ktk hilo ambalo wewe wajivunia kwalo
Km ni elimu mali cheo uzur ujuzi n.k wapo waliokuzidi kiasi huwezi hata kuwakaribia
Maisha ya duniani tunategemeana a*o hili ana lile
Kila mmoja ana umuhimu wake asiekufaa kulima atakufaa kuvuna
Majivuno dharau kujiona n.k havita kusaidia utakapofikwa na mtihani
Thamani ya gari lako la kifahari haitaonekana ukinasa ktk matope na yule anaetembea kwa miguu ndie atakaekuwa msaada kwako
Sote ni sawa tunatakiwa kula tukashiba kuvaa tukasitirika kutibiwa tukiumwa
Hata iwe tutatofautiana ktk namna ya kumaliza shida zetu lakini bado sote ni sawa mbele ya alietuumba kwa muktdha wa kuwa ni binadamu tumetokana na maji tutakwenda kuwa vumbi
Amini usiamini ila
SIKU WATOTO WAMEJAZA MAKOPO UWANJANI KWAKO NAWE UMECHOKA NDIPO UTAKAPOONA UMUHIMU WA CHIZI🚶🚶🚶🚶🚶🚶
07/07/2020
Usilazimishe mwendo ikiwa wewe ni kinyonga wahi kuanza safari mapema usisubiri kuanza safari na farasi atakuacha njiani
Kusota na kukimbia zote ni njia za kujongea muhimu ufike kwa wakati wako sahihi
Ukiona mwenzako amewahi kufika usiwe na pupa nawe muda wako wa kufika utafika tuu
Huenda aliyekutangulia amepitia magumu ambayo lau nawe ungeyapitia yangeondoa uhai wako
KILA UKIONACHO KINA UTAMU NA UCHUNGU CHAGUA KITU AMBACHO UCHUNGU WAKE UNAFAIDA
06/07/2020
MFATILIA MAKOSA YA WATU HUTUMBUKIA KTK MAKOSA MENGI NA HUZUNI NYINGI
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Contact the business
Telephone
Website
Address
Dar Es Salaam
Opening Hours
| Monday | 08:00 - 18:00 |
| Tuesday | 08:00 - 18:00 |
| Wednesday | 08:00 - 18:00 |
| Thursday | 08:00 - 18:00 |
| Saturday | 08:00 - 18:00 |
| Sunday | 08:00 - 19:00 |