Afya kwetu
Nawasaidia Watu wote wenye changamoto za uzazi bila Gharama yoyote ile.
17/04/2025
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
0755-490708
Viashiria hivi huweza kuwekwa katika makundi kutegemeana na aina ya kisukari:
a) KISUKARI KINACHOTEGEMEA INSULINI
🍁Kurithi katika familia
🍁Magonjwa ya kongosho (k**a saratani au uambukizo) ambayo huweza kuua
seli zinazotengeneza kichocheo cha insulini
🍁Mtoto kupewa maziwa mbadala (ya kopo au ya wanyama) au kumnyonyesha
mtoto kwa muda mfupi
🍁Mtoto akizaliwa na uzito mkubwa kupita kiasi
🍁 Unene au uzito mkubwa utotoni.
b) KISUKARI KISICHOTEGEMEA INSULINI
🍁 Uzito uliozidi na unene uliokithiri
🍁Shinikizo kubwa la damu
🍁Mtindo wa maisha usiofaa hususan kutokufanya mazoezi, ulaji wa vyakula
vyenye mafuta mengi na uvutaji sigara na bidhaa nyingine za tumbaku
🍁Kuwepo kwa historia ya kisukari katika familia
🍁Umri zaidi ya miaka 45.
🍁Kutokana na mabadiliko ya mtindo wa maisha, vijana wengi wamekuwa na uzito
mkubwa pamoja na kutofanya mazoezi hali ambayo inafanya tatizo hili
kuongezeka katika umri mdogo.
c) KISUKARI CHA MIMBA
KUWEPO NA HISTORIA YA KUWA NA KISUKARI KATIKA FAMILIA
🍁Kuwahi kujifungua mtoto mwenye uzito mkubwa;
🍁Mimba kuharibika mara kwa mara;
🍁 Historia ya kisukari cha mimba;
🍁 Mkojo kuwa na sukari mara kwa mara;
🍁Kuzaa mtoto mwenye ulemavu (congenital anomalies)
🍁Kuzaa mtoto mfu;
🍁Uzito au unene uliokithiri
🍁Shinikizo kubwa la damu la muda mrefu;
🍁Umri zaidi ya miaka 35.
DALILI ZA UGONJWA WA KISUKARI
0755-490708
Dalili za ugonjwa wa kisukari ni pamoja na:
🍀Kukojoa mara kwa mara
🍀Kuhisi kiu sana;
🍀Kuhisi njaa sana
🍀Kuhisi uchovu wa mwili na kukosa nguvu bila ya kufanya kazi
🍀Kupungua kwa uzito wa mwili, na kuwa mdhaifu
🍀Kutoona vizuri
🍀Kuhisi kizunguzungu
🍀Kuwa na maambukizi ya ngozi na vidonda visivyopona haraka
🍀Baadhi ya viungo vya mwili k**a vidole vya miguu na mikono kufa ganzi.
🍀Wanawake kuwashwa ukeni
🍀Kupungua nguvu za kiume/Hamu ya kujamiana kwa wanawake
🍀Miguu kuoza, vidonda au majeraha yasiyopona haraka.
🍀Majipu mwilini.
K**a una dalili hizi unapaswa kupima Kisukari.
0755-490708
Click here to claim your Sponsored Listing.
Category
Telephone
Address
Dar Es Salaam
Opening Hours
| Monday | 08:00 - 17:30 |