ummu Hawaa pedi salama

ummu Hawaa pedi salama

Share

Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from ummu Hawaa pedi salama, Health/Beauty, Bububu, Zanzibar.

26/12/2022

Jinsi ya Kuhesabu Siku za Mzunguko wa Hedhi
Siku ya kwanza ya mzunguko ni siku ambayo unapata hedhi katika mwezi husika. Siku zote kati kuanzia siku ya kwanza ya hedhi mpaka siku ya ovulation (yai kutolewa) huitwa follicular phase. Kipindi hiki kikawaida huchukua siku 14 lakini hutofautiana kati ya mwanamke na mwanamke.

Luteal phase ni kipindi kati ya ovulation(siku ambapo yai limetolewa) na siku ya kwanza kupata hedhi katika mwezi,ni katika kipindi hiki ambapo yai lililorutubishwa hujishikiza kwenye ukuta wa uterus. K**a kipindi (luteal phase) kitakuwa kifupi sana chini ya siku 12 basi itakuwa ngumu kwa kiumbe kujishikiza kwenye ukuta.

24/12/2022

Hatua za Mzunguko wa hedhi
Follicular phase
Sehemu ya ubongo inayoitwa hypothalamus hutambua kiwango cha estrogen na progesterone ambacho huzalishwa na ovari. K**a kichocheo cha estrogen kikipungua ndani ya mzunguko wa hedhi basi ubongo hutoa GnRH ambayo huamrisha pituitari kuzalisha FSH . FSH inachochea kuanza kukua kwa mayai kuanzia 10 mpaka 20.

Kati ya haya ni yai moja pekee ambalo hukomaa na kuwa tayari kurutubishwa ndani ya mwezi husika. Kadiri mayai madogo yanavokuwa huzalisha homoni ye estrogen ambayo kazi yake ni kuimarisha na kuundaa ukuta wa uterus ili kupokea kiumbe baada ya urutubishaji kufanyika.

Kadiri kiwango cha estrogen kinavyopanda ndivyo mwanamke ataanza kupata ute mzito wa rangi ya maziwa. Kuongezeka kwa kiwango cha estrogen huchochea utolewaji wa GnRH kutoka kwenye ubongo ambayo huchochea FSH na LH kwa wingi. Homoni hizi mbili huchangia utolewaji wa yai kwenye kikonyo chake kitendo hiki huitwa ovulation. Baada ya ovulation kiwango cha FS na LH huanza kupungua taratibu.

Luteal phase
Kutolewa kwa yai inafuatiwa na hatua hii ya luteal phase. Kabla ya kuendelea nataka ufahamu baadhi ya misamiati: Kumbuka baada ya yai kutolewa kwenye kikonyo linabaki kovu k**a shimo. Kovu hili huitwa corpus luteum. Kazi yake ni kuendelea kuzalisha progesterone na kiwango kidogo cha estrogen.

Ukuta wa juu mwembamba wa uterus ambao humomonyoka tunauita endometrium. Kwahivo baada ya yai kutolewa progesterone inasaidia kuendelea kuurutubisha ukuta(endometrium) ili uweze kupokea kiumbe.
Endapo hapatawepo na mbegu ya kiume(sperm) kurutubisha yai basi ukuta wa endometrium huanza kubomoka na kutolewa nje k**a hedhi.

Kwa maelezo zaidi
0776222254

24/12/2022

Homoni hizi mbili yaani LH na FSH hulenga kuamrisha ovari kuzalisha homoni za estrogen na progesterone. Ovari napenda kuita ni kiwanda cha kuzalisha na kuhifadhi mayai. Fikiria homoni hizi zinafanya kazi k**a vile mfano wa vitabu vilivyopangwa mezani kwa wima vikilaliana, ikitokea kitabu cha mwanzo kimeondolewa kwenye mstari basi vyote vinaanguka.

Ni mlolongo mrefu na k**a ikitokea mvurugiko wa homoni moja basi mtiririko wote unaharibika na unaanza kukosa hedhi au hedhi kuvurugika, na matatizo mengine mengi ya uzazi ikiwemo uvimbe na ugumba. Zifuatazo ni hatua za mzunguko wa hedhi.

22/12/2022

Mwongozo wa hedhi salama
Hedhi salama ni ipi
mzunguko wa hedhi
Kwa mwanamke kuwa na mzunguko mzuri wa hedhi ni jambo la kujivunia na linaloleta heshima sana. Mzunguko wa hedhi unaweza kutoa picha kamili nini kinaendelea kwenye mwili wa mwanamke. K**a mfuko wa mimba unapata mzunguko mzuri wa damu, homoni zako zinbalansi, au k**a mayai yanatolewa kwenye ovari.

Hedhi ni kitu gani?
Hedhi ni muunganiko wa yai ambalo halikurutubishwa pamoja na damu inayotokana na kumomonyoka kwa tishu laini za ukuta wa mfuko wa mimba (uterus). Kitendo hiki hutokea kila mwezi kwa mwanamke.

Jinsi mwili unafofanya kazi mpaka kupatikana kwa hedhi
Kupata hedhi ni kitendo kinachoratibiwa na mzunguko wa homoni. Kwa maelezo mafupi na rahisi ni kwamba inaanza na eneo la ubongo linaloitwa hypothalamus kuzalisha homoni ya gonatrophin (GnRH) ambazo zinachochea tezi ya pituitary kuzalisha homoni ya luteinizing(LH) na Follicle stimulating hormone(FSH).

21/12/2022

Jinsi ya kukabiliana na uchungu wa hedhi.

Baadhi ya wanawake huwa na uchungu mwingi sana kwasiku moja au mbili wakati wa hedhi. Anaweza kutumia dawa za kupunguza uchungu k**a ibuprofen au paracetamol. Pia anaweza kutumia chupa ya maji moto mahali penye uchungu na amuone daktari au apate usaidizi kwa kituo cha kupanga uzazi jinsi ya
kumudu uchungu.

Kukabiliana Na Hedhi.

Mwanamke akiwa na hedhi anapaswa kutumia vis**o au pedi kuzuia damu. Pedi zimeundwa na vifaa vya laini zinazo nyonya damu. Pedi hupachikwa na kukwama ndani ya chupi. Pedi zipo za ukubwa tofauti ili kumsaidia yeyote mwenye hedhi nyepesi au nzito.
Kuna wanawake ambao hupenda visos kushinda Pedi.
S**o ni kifaa chenye umbo la mche kitumiwacho na wanawake sehemu za ukeni ili kuzuia damu wakati wa hedhi.
S**o huwa na u*i unaosaidia kuvutwa nje kwa urahisi. Unapaswa kubadilisha s**o na pedi mara nne kwa siku au zaidi kutegemea
na u*ito wa hedhi. Unapobadilisha, ifunge kwenye shashi kisha uweke kwenye jaha au Kwa zile za kutumia zaidi ya mara moja hakikisha unaisafisha vyema na kuikausha vizuri kabla ya kutumia tena.
Usiwahi kutupa s**o kwenye vyoo vya maji
kwa sababu vitaziba.

20/12/2022

Je Hedhi Ni Nini?

Hedhi ni baadhi ya mabadiliko katika mwili wa wanawake ambayo hutayarisha nyumba ya uke kupata ujau*ito. Kila mwezi mji wa
uzazi hupata kokwa ambapo mwanamke akipata ujau*ito, mtoto ataweza kukuwa.. Mwanamke asipo pata ujau*ito, kokwa haitajiki na damu itatokea ukeni- damu anayoipata mwanamke ambaye hana ujau*ito ni hedhi. Hapa Tanzania wanawake wengi husema
wamepata ‘hedhi’.

Hufanyika Lini?

Wanawake wengi walio komaa hupata hedhi. .Wasichana hupata hedhi zao kati ya miaka 9 na miaka 16. Wanawake huacha kupata hedhi wanapotimia miaka 50. Hedhi huchukua siku tatu hadi saba kila mwezi. Wanawake wengine hupata hedhi nyepesi ,wengine nzito na za uchungu.
Ukiona tatizo juu ya hedhi, muone daktari
au kituo cha upangaji wa uzazi.

Miongoni mwa city muhimu ya kukusaidia kipindi cha hedhi no kuangalia usafi wako na Sisi tupo Kwa Hilo la usafi ili kuhakikisha unajilinda na maradhi mbali mbali. Tafadhali wasiliana nasi tukusaidie...
0712423242
Jioni njema

19/12/2022

Karibu ummu Hawaa pedi salama tukuhudumie
Tunatengeneza na kuuza pedi salama Kwa usalama wa afya yako.
Unajiskiaje kutumia kifaa cha usafi unachokijua usafi wake ukilinganisha na usichokijua?!....

Want your business to be the top-listed Beauty Salon in Zanzibar?
Click here to claim your Sponsored Listing.

Category

Telephone

Website

Address


Bububu
Zanzibar

Opening Hours

Monday 09:00 - 17:00
Tuesday 09:00 - 17:00
Wednesday 09:00 - 17:00
Thursday 09:00 - 17:00
Friday 09:00 - 12:00
Saturday 09:00 - 17:00
Sunday 09:00 - 17:00

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ummu Hawaa pedi salama posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Subscribe

We will notify you when anything happens in Zanzibar.